wanamitindo wanaochipukia nchini wametakiwa kujitambua pamoja na kuwa
na mikakati ya kujitangaza zaidi ili kupata soko la ndani na nje ya nchi.
Wito huo ulitolewa jana na Mwanamitindo mahiri wa mavazi nchini Sheria
Ngowi wakati akizungumza na Wanamitindo kutoka kampuni ya Black Fox Model
Africa.
Ngowi pamoja na mtaalamu wa urembaji Edna Ndibarema wa kampuni ya Ndiba
Style walialikwa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, ya Black Fox Model Africa, Aj
Mynah kuzungumzia fursa zilizopo katika tasnia hiyo.
Ngowi aliwataka wanamitindo kuichukulia kazi hiyo kuwa ni sawa na kama
kazi nyingine zenye kipato licha ya kuwa kwa hapa nchini ni fani ambayo inazidi
kukua kwa kasi.
Alisema kuwa akiwa kama mwanamitindo ametembea nchi mbalimbali kuonesha
mavazi na amekutana na wanamitindo mbalimbali wa kimataifa ambao walianza
kufanya kazi hiyo wakiwa kama wanamitindo wa kawaida.
Alisema kuwa ili wanamitindo wa Tanzania nao kufikia hatua kama hiyo
wanatakiwa kuwa na mikakati mingi ya kujitangaza ambapo aliwataka kutumia zaidi
vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kujitangaza.
Sheria Ngowi akiwafunda somo wanamitindo
Alisema kwa kwa kutumia mitandao kama Twiter, Facebook, Instagram
pamoja na tovuti nyingine mbalimbali kubwa wanamitindo wanaweza kujijengea jina
na kutumiwa na makampuni mbalimbali kutangaza biashara zao.
0 comments:
Post a Comment