Thursday, May 28, 2015

ZIJUE FAIDA ZA ASALI KWA AFYA YAKO


Asali ni kimiminika chenye ladha tamu ya sukari, chenye kunata na rangi ya manjano. Asali kama chakula na dawa ni dhana kongwe katika historia ya mwanadamu. Kwa mfano yapata miaka 4,000 iliyopita madaktari wa tiba wa Kimisri na wale wa Sumarani waliitumia asali kutibu magonjwa mbalimbali kama vile vidonda vya tumbo na vile vya kawaida, magonjwa ya macho, ngozi na yale ya tumbo.
Faida za asali kiafya


1. Asali hutumika kama chakula hivyo huongeza nguvu mwilini.


2. Ni kiongezeo katika vyakula kama mkate, karanga na nafaka nyingine.


3. Hutibu vidonda mbalimbali (kama vidonda vya kuungua na moto, mikwaruzo kwenye ngozi n.k)



4. Kwa kunywa mchanganyiko wa asali, siki na maji katika vipimo sawa ni tiba kwani huaminika kuua vijidudu visababishavyo magonjwa.

5. Hufanya ngozi yako kuwa nyororo na katika hali nzuri isiyo ya ukavu wakati wote. Paka asali kwenye ngozi na acha kwa dakika 30 kisha jisafishe. Fanya hivyo mara kwa mara na utaona mabadiliko katika ngozi yako.


6. Asali huboresha na kuweka nywele katika hali nzuri wakati wote (natural hair conditioner). Changanya kijiko kimoja cha asali na shampoo kisha tia mchanganyiko huo kwenye nywele zako kwa dakika 20, osha na kausha nywele zako vizuri.


7. Huondoa chunusi na kuboresha ngozi yako. Paka asali sehemu yenye chunusi kwa dakika 30 kisha osha ngozi yako kwa maji ya vuguvugu. Fanya hivyo kwa siku kadhaa utaona mabadiliko.


Matumizi ya asali katika matibabu


Sehemu nyingi duniani watu wanatumia asali kutibu magonjwa mbalimbali. Licha ya kuwa asali huongeza kinga ya mwili, sayansi ya tiba imebaini asali bora ina wingi wa sukari (76g/ml), tindikali (acidity, Ph = 3.6-4.2) na baadhi ya kemikali ambazo zinatokana na viumbe hai (organic compounds) vyote kwa pamoja ni sababu za asali kuwa ni dawa. 


Virutubisho vya kiafya katika asali

  • Asali ni chanzo cha sukari hivyo mwili hupata nguvu na nishati. 
  • Asali inamchanganyiko wa virutubisho na kemikali za aina mbali mbali. Baadhi ya vitu hivyo ni sukari, vitamini, amino acids (vitu vinavyotengeneza protini), vimeng'enyo (enzymes)
Kwa hayo machache kuhusu asali na matumizi yake naamini utakuwa umefaidika kwa kujua mambo kadha wa kadha kuhusu asali. Tumia asali kama kinga na tiba ya mwili wako.

0 comments:

Post a Comment